1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Rais Assad achukua kipindi cha pili cha uongozi

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBho

Rais Bashir al Assad wa Syria anaapishwa hii leo kuendelea na kipindi cha pili cha urais, huku nchi hiyo ikikabiliwa na chagizo kubwa kutoka Marekani juu mzozo wa Lebanon na Iraq.

Assad ambaye alipata ushindi wa asilimia 97, katika kura ya maoni mwezi wa tano, ambapo alikuwa mgombea pekee, anatarajiwa kulihutubia bunge na kuelezea sera zake za ndani na nje.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 41 aliingia madarakani mwaka 2000 baada ya kifo cha baba yake Hafez al Assad ambaye aliiongoza Syria kwa mkono wa chuma kwa miongo mitatu.

Marekani imeitaka Syria kuacha kuingilia mambo ndani ya Lebanon, na inailaumu kwa kushiriki katika kuiweka hali tete Iraq.