1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Syria na Iraq zakubaliana kupambana na ugaidi

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiK

Syria na Iraq zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika kupambana na ugaidi na uhalifu.

Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi hizo mbili walitia saini hapo jana makubaliano hayo huko mjini Damascus Syria.

Syria na Iraq pia zimesema zinataka kuunda mfumo wa maendeleo kwa ajili ya kulinda maeneo ya mipaka yao.Hatua hii imekuja wakati ambapo kwa mara nyingine Syria imeanza kukosolewa kwamba inawarahisishia wapiganaji wa kigeni kuvuka mpaka na kuingia Iraq.