1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Syria yailamu Marekani kuingilia siasa za Lebanon

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7ER

Syria inailaumu Marekani kwa kuingilia siasa za ndani za Lebanon na kuegemea upande mmoja jambo linalohatarisha usalama wa Lebanon.Katika waraka uliofikishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na kuchapishwa na shirika la habari la taifa.. Syria inaheshimu taifa la Lebanon na uhuru wake na haiingilii kati uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Marekani inaunga mkono serikali ya Lebanon inayoongozwa na Fouad Siniora inayokabiliwa na mkwamo wa kisiasa na vyama vya upinzani vinavyoongozwa na kundi la Kishia la Hezbollah.Kundi la Hezbollah ni mwandani wa Syria na Iran.

Kwa upande mwingine Syria inasema iko tayari kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Lebanon punde uongozi nchini humo utakapobadilika.