1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damu inazidi kumwagika nchini Irak licha ya mpango mpya wa usalama

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBM

Baghdad:

Watu wasiopungua 17 wameuwawa bomu lililofichwa ndani ya gari liliporipuka huko Mahmudiya-umbali wa kilomita 30 kusini mwa Baghdad.Meya wa mji huo MUAID Al Amari amesema jumla la ghorofa tatu ,maduka na magari yaliyokua karibu na hapo yameripuliwa.Wakati huo huo wanajeshi wanne wa kimarekani wameuwawa jana gari yao iliporipoliwa kwa mabomu njiani kaskazini mwa Baghdad.Mashambulio haya yanasadifu katika wakati ambapo serikali ya Irak imetia njiani mpango mpya wa usalama kwa lengo la kuwavunja nguvu waasi na kuepusha balaa la kutumbukia katika janga la vita vya wenyewe kwa wenyewe.Wakati huo huo maelfu ya washiya waliosheheni ndani ya magari wanaelekea Nadjaf,wakiitika mwito wa Imam Muktada el Sadr wa kuadamana kesho dhidi ya Marekani katika mji huo wa kusini mwa Irak.Mashahidi wanasema polisi wanajaribu kuwazuwia wafuasi wa Muktada el Sadr wasishiriki katika maandamano hayo-kuadhimisha miaka minne tangu vikosi vya Marekani vilipoivamia Irak.