1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damu inazidi kumwagika nchini Irak

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs7

Baghdad:

Mahabusi wasiopungua 70 kati ya watu 150 waliotekwa nyara mapema wiki hii mjini Baghdad hawajulikani waliko-baadhi yao wameuliwa na wengi wameteswa-amesema waziri wa elimu ya juu Abed Diab al Oujaili aliyezisuta na kukosoa moja kwa moja hoja za waziri mkuu Nouri El Maliki.Waziri al Oujaili anasema mahabusi walioachíwa huru ndio waliowaambia kuna wenzao waliouliwa na wengine walioteswa.Bwana al Oujail amejiuzulu kwa muda na anasema hatorejea serikalini si mpaka mahabusi wote wameachiliwa huru.Katika mahojiano na kituo cha matangazo cha BBC waziri huyo wa elimu ya juu amesema anahisi kana kwamba hakuna serikali nchini Irak.Waziri wa elimu ya juu anasisitiza anataka wateka nyara wakamatwe kabla ya kurejea serikalini.Kisa cha utekaji nyara kimejiri licha ya maelfu ya polisi wa Irak na wanajeshi wa Marekani wanaopiga doria mjini Baghdad.Wakati huo huo damu inaendelea kumwagika katika mji mkuu huo wa Irak ambako watu 14 wameuliwa leo asubuhi huku jeshi la marekani likisema wanajeshi wake kumi wameuwawa tangu jumanne iliyopita mjini humo na katika maeneo ya karibu na hapo.