1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Mradi wa kupunguza bei za dawa za malaria

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgC

Rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton anazindua mradi wa kusaidia kulipia dawa za malaria nchini Tanzania.Mradi huo unafanyiwa jeribio ikitarajiwa kuwa utaweza kuwa mfano mzuri kwa bara zima la Afrika.Kuambatana na mradi huo,dawa za malaria za ACT zinatazamiwa kuwa rahisi kwa asiliamia 90 kulinganishwa na bei ya hivi sasa.