1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM : Tume ya suluhu kuanza kazi Burundi

25 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgH

Tume ya kusimamia suluhu ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Burundi na kundi la mwisho la waasi lililokuwa limebakia nchini humo la FNL itaanza shughuli zake mwezi ujao.

Tume hiyo ya Pamoja ya Kuyakinisa na Kufuatilia suluhu hiyo ambayo imechelewa mno kuanza kazi inatazamiwa kwenda nchini Burundi mwezi ujao kuanza kazi yake.

Tume hiyo ambayo imeundwa hapo Oktoba Mosi inaundwa na maafisa kutoka Burundi,Afrika Kusini,Tanzania,Uganda,Umoja wa Mataifa na FNL.Tume hiyo ambayo kazi yake ilikwama kutokana na waasi kususia kushiriki inatazamiwa kuangalia utekelezaji wa usitishaji wa mapigano uliotiwa saini hapo mwezi wa Septemba mwaka 2006.

Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya masuala ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Tanzania Joram Biswaro viongozi wa FNL hapo Ijumaa walikabidhiwa hati ya msamaha iliosainiwa na Rais Piere Nkuruzinza ambayo itawawezesha kurudi nchini Burundi bila ya kushtakiwa.