1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM : Waanglikana wajadili msimamo juu ya ushoga

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRv

Viongozi wa Wakristo wa madhehebu ya Kianglikana milioni 77 duniani leo wanakutana mjini D’salaam kujadili hatua ya kuregeza msimamo juu ya mashoga iliochukuliwa na tawi la kanisa hilo nchini Marekani wakati wasi wasi wa kuwepo kwa wachungaji mashoga na ndoa za jinsia moja ukitishia kuligawa kanisa hilo.

Viongozi wa kanisa hilo kutoka majimbo yake makuu 38 duniani watakuwa na mkutano wa faragha wiki hii na suala la msimamo wa Marekani kwa mashoga liko juu katika agenda.

Hitilafu baina ya Waanglikana zimekuwa zikizidi kuongezeka kwa miaka sasa na kuja kuwa mzozo wakati tawi la kanisa hilo nchini Marekani Kanisa la Episcopal lilipomtawaza askofu wake wa kwanza shoga wa kujitangazia.