1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daraja laporomoka na kuua zaidi ya watu 10

25 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Cg9s

KATHMANDU

Zaidi ya watu 10 wamekufa na wengine wengi hawajulikani waliko baada ya kuporomoka kwa daraja iliyokuwa na msongamano wa watu nchini Nepal.

Polisi wanasema watu hao walikuwa wakipita kwenye daraja hilo katika kijiji cha Chunchu kiasi kilomita 500 kutoka mji wa Nepal Kathamandu wakati lilipoporomoka.

Taarifa zinasema baada ya kuporomoka kwa daraja hilo watu wengi walijaribu kuogelea kwenye mto Bheri lakini idadi ya waliokufa inatazamiwa kuongezeka.