1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARFUR:Umoja wa mataifa walaani kutekwa kwa wafanyikazi wake

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5O

Umoja wa mataifa umelaani kukamatwa kwa wafanyikazi wake sita wa mashirika ya kutoa msaada katika jimbo la mgogoro la Darfur.

Mratibu wa masuala ya misaada ya kiutu katika Umoja huo Manuel Aranda Da Silva ameonya kwamba vitendo kama hivyo vinahatarisha shughuli za kibinadamu kwenye eneo hilo.

Wafanyikazi hao wanaofanya kazi na shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR walikamatwa katika eneo la Um Shalaya magharibi mwa jimbo la Darfur.

Watu waliokuwa na bunduki waliwateka nyara na kuwatelekeza jangwani.Walionekana baada ya kufanywa opresheni kubwa ya kuwatafuta iliyoongozwa na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika.