1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

David Cameron anaelekea kuwa mshindi

Admin.WagnerD8 Mei 2015

Matokeo ya utabiri wa awali yanaonesha chama cha waziri mkuu David Cameron cha Conservative kwa mshangao mkubwa kikipata viti vingi katika uchaguzi huo uliofanyika jana(07.05.2015) nchini Uingereza.

https://p.dw.com/p/1FMbH
Großbritannien Wahl zum Unterhaus Ergebnis Die Konservativen David Cameron
David Cameron , waziri mkuu wa UingerezaPicha: Reuters/T. Melville

Matokeo hayo ya utabiri wa awali yanaashiria kwamba David Cameron yuko karibu kabisa na kuunda serikali mpya.

Chama cha upinzani cha Labour hakijafanya vizuri katika uchaguzi huu kuliko ilivyotarajiwa, matokeo ya awali ya utabiri yanaonesha , na mshirika wa chama cha waziri mkuu David Cameron katika serikali ya mseto, chama cha Liberal democrats, kimetayarajiwa kupoteza vingi ya viti vyake.

Großbritannien Wahl zum Unterhaus Ergebnis Labour Ed Miliband
Ed Miliband kiongozi wa chama cha LabourPicha: Getty Images/M. Lewis

Matokeo mazuri zaidi yamepatikana kwa chama kinachotaka kujitenga kwa Scottland chama cha Scottish National , ambacho kinaonekana kupata viti vyote isipokuwa kimoja tu katika Scottland.

Matokeo hayo ya awali , yaliyopatikana kutokana na mahojiano na wapigakura 22,000, yamepingana kwa kiasi kikubwa na uchunguzi wa awali wa maoni ya wapiga kura uliofanywa wakati wa kampeni za mwezi mzima, ambao umekipa chama cha Cameron cha Conservative na chama cha Labour cha Ed Miliband kuwa vinafungana kwa kugawana kiasi ya theluthi moja ya kura.

Großbritannien Wahl zum Unterhaus Ergebnis SNP Nicola Sturgeon
Nicola Sturgeon kiongozi wa chama cha SNPPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Heppell

Matokeo ya utabiri wa awali yalionesha kwamba chama cha Conservative kitapata viti 316, ikiwa ni ongezeko kutoka viti 302 na vingi zaidi kuliko ilivyotabiriwa, na chama cha Labour kitapata viti 239 ikiwa ni chini kutoka viti 256. Chama cha Liberal Democrats kitapungukiwa kutoka viti 56 hadi viti 10 tu, na chama cha Scottish nationalists kitapanda kutoka viti sita hadi 58.

Iwapo makadirio hayo ni sahihi , chama cha Conservative kitakuwa katika nafasi ya mbele kuunda serikali ijayo kwa kuomba ushirika na vyama vidogo.

Wapiga kura wavikimbia vyama vikuu

Chama cha Conservative na Labour vimeshuhudia uungwaji mkono ukiporomoka wakati wapiga kura wanageukia vyama vingine, hususan kwa chama cha Scottland Nationalists, chama ambacho kinakuwa na uungwaji mkono mkubwa upande huo wa kaskazini , na chama kinachopinga wahamiaji cha U.K Independence Party.

Wahl in Großbritannien: Auszählung der Stimmen in Glasgow, Scotland, am 07. Mai 2015
Zoezi la kuhesabu kura likiendeleaPicha: picture-alliance / ZUMA Press

Wanasiasa wa chama cha Conservative hawajatangaza ushindi na Labour hakijakubali kushindwa, wakati kila kimoja kinasubiri kuona iwapo utabiri huo utakuwa kweli.

Siku nzima jana katika taifa hilo lenye wakaazi milioni 64 , wapiga kura walimiminika katika mashule, makanisa na hata vilabu vya pombe kutoa kauli yao kuhusiana na hali ya baadaye ya taifa lao.

Großbritannien Wahlen
Wapiga kura wakielekea kupiga kuraPicha: DW/B. Wesel

"Huu ni uchaguzi wenye shauku kubwa kwa kadiri ninavyokumbuka," amesema Lesley Milne, mwenye umri wa miaka 48 kutoka Glasgow, na ambaye anakiunga mkono chama cha Scottish National.

Muda umefika kuwatikisa wanasiasa mjini London na chama cha SNP ndio wanaoweza kufanya hivyo.

Mhariri: Daniel Gakuba