1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAVOS: Mzozo wa Mashariki ya Kati wagusiwa mjini Davos, Uswisi.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXx

Jitihada za kufufua mashauriano ya amani ya Mashariki ya Kati zimedhihirika siku ya pili ya kikao cha dunia cha uchumi, World Economic Forum, kinachoendelea mjini Davos, Uswisi.

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, amekutana na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, pembeni mwa mkutano huo ingawa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu mashauriano yao.

Mapema kabla ya mkutano huo, Rais Mahmoud Abbas, aliwaambia waandishi wa habari anatarajia Ujerumani itajihusisha zaidi kwenye suala hilo hasa kwa kuwa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya pamoja na kundi la mataifa manane yaliyostawi kiviwanda.