1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAVOS:Mkutano wa dunia wa kiuchumi wamalizika Uswisi.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWz

Mkutano wa dunia wa kiuchumi, World Economic Forum, umemalizika mjini Davos, Uswisi, kwa wingi wa matumaini ya kushughulikiwa maswala kadhaa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, bara la Afrika na pia hali ya biashara duniani.

Mataifa makubwa yamekubaliana kuanza tena duru ya Doha iliyokwama ya mashauriano ya biashara.

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, wamesisitiza haja ya kuendelea na duru ya Doha ili kuhakikisha biashara imefanywa kuwa huru.

Mzozo wa Mashariki ya Kati pia ulishughulikiwa kwa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas na Makamu Waziri Mkuu wa Israil, Tzipi Livni kuelezea nia yao kuhakikisha kuwepo mataifa mawili huru kati ya Palestina na Israil.