1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Demnjanjuk

Abdu Said Mtullya21 Aprili 2009

Wizara ya sheria ya Marekani yasema John Demnjanjuk anaweza kutimuliwa Marekani.

https://p.dw.com/p/Hb26
Mahakama ya Ujerumani yamsubiri mtuhumiwa Demnjanjuk.Picha: AP

CINCINATTI.

Wizara ya sheria ya Marekani imeiagiza mahakama ya Cincinatti iondoe kipengere cha sheria kinachozuia kutimuliwa  Marekani, kwa John Demnjanjuk anaetuhumiwa kuhusika na maangamizi ya wayahudi alfu  29  wakati wa vita kuu vya pili.

Mtuhumiwa huyo alikuwa mlinzi kwenye kambi ambapo mafashisti waliwafunga na  kuwaangamiza wayahudi.

Mtu huyo anatakiwa afikishwe mbele ya mahakama , nchini Ujerumani ili   ajibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Lakini kuletwa  Ujerumani  kwa Demnjanjuk kumekuwa  kunaahirishwa mara  kwa  mara na  mahakama  ya Marekani.