1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Deutsche Welle kutoa mafunzo kwa njia ya radio.

Sekione Kitojo14 Novemba 2007

Ujerumani Frank-Walter Steinmeier analiona bara la Ulaya kuwa linawajibu tu wa kuisaidia Afrika . ameyasema hayo katika mktano wa mabalozi wa nchi za Afrika mjini Berlin , mkutano ambao shirika la utangazaji la Deutsche Welle liliwaalika. Amefurahishwa zaidi na ukweli kwamba mwezi wa Desemba baada ya miaka saba hatimaye kutafanyika mkutano baina ya mataifa ya Ulaya na Afrika. Steinmeier pia amezungumzia uungaji mkono wake kwa radio Deutsche Welle katika mradi wake wa elimu kwa njia ya radio kwa ajili ya Afrika, baada ya Deutsche Welle kuutangaza rasmi mradi huo. Ripoti ya Peter Stützle.

https://p.dw.com/p/CHj7

Katika ukumbi ambao ulijaa mabalozi kadha kutoka mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara , walimsikiliza mkuu wa idara ya idhaa za Kiafrika ya radio Deutsche Welle Ute Schaeffer, akiwahubiria huku kukiwa na picha ya wasichana kutoka Afrika katika kiwambo cha televisheni nyuma yake.

Tunataka kwa mfano kutoa elimu ya kazi. Ndoto ya msichana huyu kutoka bara la Afrika , Esther, ni kuwa muuguzi katika hospitali. Haya ni maelezo ya kazi anayoipenda. Tutafanya hivyo kutokana na maelezo na mahojiano, na sio kwa kutumia vipindi tofauti tofauti, lakini katika umbo ambalo wasikilizaji wetu vijana wanalitarajia na kilichotayarishwa kwa ajili yao.

Wazo la kuwa na mafunzo kwa njia ya radio kwa ajili ya vijana katika lugha za Kiafrika , linatokana na washirika wetu Deutsche Welle katika bara la Afrika. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier analikubali hili vizuri kabisa. Na anataka kuliomba bunge kuidhinisha mamilioni ya Euro kwa mahitaji hayo ya elimu kwa Afrika. Baadhi ya mataifa ya Afrika yanapiga hatua kubwa za kiuchumi, amesema Steinmeier, hususan anaona binafsi mabadiliko ya msimamo kwa viongozi wa serikali, kutaka kuwajibika kutatua matatizo ya nchi zao.

Na kwasababu ninaliona hilo, nahisi kuwajibika kusema kuwa ni wangapi kati ya wenzangu katika bara la Ulaya , ambapo mabadiliko haya endelevu yanayotokea katika Afrika wataweza kuyaunga mkono, kama tulivyoweza kufanya hapo nyuma.

Na mfumo wa msaada huu endelevu , amesema Steinmeier utakuwa ni kwa njia ya elimu kwa watoto na vijana . Hii ni muhimu kwa Afrika kama ilivyo kwa Ulaya.

Bila elimu ni hakika kabisa kuwa hakutakuwa na ukuaji wa uchumi, bila elimu hakuna nafasi sawa kwa jamii, bila ya elimu hakuna ushiriki wa kisiasa.

Muhimu kwa maendeleo sahihi hususan , ni kwamba Waafrika wengi wawe na uwezo sio tu wa kumaliza elimu ya msingi , amedokeza Steinmeier. Kwa kuwa idadi kubwa ya watoto na vijana wa Kiafrika hawapati nafasi ya elimu ya juu, radio inaweza kuchukua nafasi muhimu. Kwa hilo Ute Schaeffer kutoka Deutsche Welle hakuwa na lingine ila kukubaliana.

Radio katika Afrika kama ilivyokuwa hapo zamani, ni chombo muhimu , ambapo inapatikana kila mahali, na mtu hahitaji utaalamu mkubwa. Na katika hilo inawezekana kutoa maelezo ya elimu, na pia naweza kusema, inafurahisha, taarifa zikitumwa kupitia radio, mtu anaweza kupata maarifa mkubwa. Kimsingi mtu anatarajia kupata nafasi ya kupata elimu kwa kupitia vipindi vya radio.

Mradi wa elimu wa Deutsche Welle ukiwa na kichwa cha habari , elimu kwa kutumia sikio , sio mpango uliotoka Ujerumani na kupelekwa Afrika. Waandishi wengi wenye uzoefu kutoka Afrika wameandika kuhusu hilo na pamoja na hayo hata washirika wanaorusha matangazo ya radio Deutsche welle wameweza kutayarisha vipindi kama hivyo.