1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Deutsche Welle yamtunukia mkuu wa uchaguzi Sierra Leone

15 Septemba 2009

Mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini Sierra Leone Christiana Thorpe amepewa tunzo na Deutsche Welle kutokana na mchango wake katika kuleta na kuimarisha demokrasia nchini humo

https://p.dw.com/p/JhGS
Mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini Sierra Leone Christiana ThorpePicha: DW

Sherehe za kukabidhiwa tuzo hiyo zinafanyika katika jengo la Deotsche Welle leo hii, ambapo wageni kadhaa wanatarajia kuudhuria ghafla hiyo.

Sierra Leone iliyoko magharibi mwa Afrika, ni nchi yenye maendeleo hafifu, pamoja na kwamba ina utajiri wa madini, kama dhahabu na almasi.Mnamo mwaka 2000, muongo mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, ulimalizika.

Hata hivyo, kutokana na kuendelea kubakia kwa vitendo vya ghasia,na umasikini, Umoja wa Mataifa ukalazimika kupeleka kikosi kikubwa kabisa cha kulinda amani kuwahi kufanya hivyo duniani.

Lakini kuanzia wakati huo mfumo wa siasa wenye kufuata misingi ya kidemokrasia umekuwa ukijikita taratibu nchini humo.Miongoni mwa waliyochangia hali hiyo ni mwenyekiti huyo wa tume huru ya uchaguzi nchini humo Bibi Christiana Thorpe.

Bibi Thorpe anapoiangalia hali ya umasikini uliyotopea nchini humo, ana matumaini kuwa hali hiyo itabadilika.Sierra Leone inakamata nafasi ya mwisho katika orodha ya Umoja wa Mataifa ya nchi masikini, lakini mwenyekiti huyo wa tume ya huru ya uchaguzi anasema hali hiyo itapanda haraka.

´´Nina matumaini makubwa sana, na nina nadhani nchi yangu inaelekea katika mafanikio, tuko imara na tutafanikiwa´´alisema.

Matumaini hayo yanatokana na juhudi kubwa anazofanya Bibi Christiana Thorpe, ambaye alikuwa mwalimu, hatimaye Waziri wa Elimu mwaka 2005, kabla ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini humo.

Tokea kuteuliwa kwake kuongoza tume hiyo, Bibi Thorpe amejijengea uadui.Vita vya wenyewe kwa wenyewe, viliacha siasa za matabaka, kama vile kuwepo kwa sheria na taratibu za kidemokrasia

Katika uchaguzi mkuu wa bunge na urais wa mwaka 2007, ulishuhudia vitendo vya kudhibiti vyombo vya habari na pia kununua wapiga kura katika jamii za watu waliyoko kwenye maeneo ya vijijini.Lakini hata hivyo Christiana Thorpe aliwahamasisha wananchi  siyo tu kufahamu juu ya haki zao, lakini pia kuitumia haki yao hiyo ya kupiga kura, kazi ambayo ni ngumu katika jamii ambako kati watu wanne watatu hawajui kusoma wala kuandika.Alifafanua kwa kusema.

´´Kama unataka mfumo wa demokrasia ufanyekazi yake vizuri, basi ni kwenda katika wananchi wa kawaida kuangalia jinsi gani watakavoweza kuanza kuelewa, kwanini wanatakiwa kupiga kura, vipi watapiga kura na kitu ganai wanachokipigia kura´´alisisitiza

Tume huru ya uchaguzi nchini Sierra Leone ndiyo maana ikapeleka mashine za kupigia mahesabu, mashuleni, katika jumuiya za kijamii na pia familia ziligaiwa.Na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, matokeo yakawa ya ajabu kiasi.

Takriban asilimia 75 ya watu walipiga kura, ambapo aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa chama cha All People's Congress (APC)  Ernest Bai Koroma alichaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Mafanikio ya mabadiliko ya uongozi  ni kutokana na kufuata misingi ya kidemokrasia na tume huru ya uchaguzi nchini humo, inayoongozwa na Christiana Thorne ndiyo yenye kustahili pongezi kwa mafanikio hayo.Umoja wa Mataifa uliupongeza uchaguzi huo wa mwaka 2007 ukiutaja kuwa ni mfano wa kuigwa katika  uimarishaji wa demokrasia.Na  kimsingi mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi nchini Sierra Leone sasa anajiandaa kuusimamia uchaguzi wa mwaka 2012.

Mwandishi:Ute Schaeffer/DW Afrika/ Aboubakry Liongo

Mhariri:M. Abdul-Rahman

bild

http://fried.dwelle.de/dwelle/cma/bild_db/preview/1,2609,J-4643118,00.html

http://fried.dwelle.de/dwelle/cma/bild_db/preview/1,2609,J-4643120,00.html

http://fried.dwelle.de/dwelle/cma/bild_db/preview/1,2609,J-4643122,00.html

E N D E