1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhaka. Kimbunga Sadr chashambulia.

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CI1h

Nchini Bagladesh mamia kwa maelfu ya wanavijiji wamekimbilia ndani ya nchi hiyo , wakikimbia kimbunga Sidr, ambacho kimeanza kushambulia eneo la pwani ya kusini mwa nchi hiyo.

Upepo umesababisha mawimbi makubwa na mafuriko katika visiwa vya nchi hiyo. Kimbunga Sidr kikiwa na upepo unaokwenda kasi ya kilometa 200 kwa saa , umelazimisha kufungwa kwa uwanja wa ndege wa Chittagong na huduma za bandari. Kimbunga hicho pia kinatarajiwa kuathiri maeneo ya jirani ya Bengal nchini India.