1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA : Maelfu wahamishwa kutokana na kimbunga

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1B

Maelfu ya wananchi wa Bangladesh na India wamehamishwa kutoka maeneo ya mwambao wakati utabiri wa hali ya hewa ukionya kwamba kimbunga kikali kiliowekwa kwenye daraja la nne kinaweza kupiga maeneo hayo baadae leo hii.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Bangladesh imesema kimbunga hicho kwa jina Sidr kinan’guruma kwenye Ghuba ya Bengal na kina nguvu ya upepo unaosafiri kwa kilomita 210 kwa saa kinaelekea maeneo ya kusini mwa Bangladesh kwenye mpaka na India.

Maafisa wa serikali wanasema kiwanja cha ndege cha Chittagong na bandari imefungwa.

Hapo mwaka 1970 takriban watu laki tano walikufa wakati kimbunga kilipopiga nchi hiyo ya kimaskini na hapo mwaka 1991 watu wanaokadiriwa kufikia 140,000 walikufa kutokana na gharika la mawimbi yaliosababishwa na kimbunga.