1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Mafuriko yachukua maisha ya watu 15

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgE

Nchini Bangladesh,si chini ya watu 15 wamepoteza maisha yao katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha siku tatu zilizopita.Vile vile,kama watu wapatao nusu milioni wamenasa majumbani mwao.

Wataalamu wa kutabiri hali ya hewa wamesema,mito mingi imefurika kufuatia mvua kubwa zilizonyesha saa 24 zilizopita.

Mafuriko yaliyotokea katika msimu wa masika mwaka huu,yameua zaidi ya watu 770 nchini India, Bangladesh,Pakistan na Afghanistan.