1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Vikosi vimesamabazwa kulinda usalama Bangladesh

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkU

Serikali ya mpito ya Bangladesh imetoa amri ya kuvisambaza vikosi katika mji mkuu,Dhaka na vituo vingine muhimu kwa azma ya kuzuia machafuko wakati wa kufanywa matayarisho ya uchaguzi wa mwezi ujao.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya upinzani kuahidi kuendelea na maandamano ya kutaka mabadiliko yafanywe katika utaratibu wa uchaguzi,ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki.Uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa aliekuwa waziri mkuu Khaleda Zia, umepangwa kufanywa Januari 23.Bibi Zia,mwisho wa mwezi Oktoba aliikabidhi madaraka serikali ya mpito inayoongozwa na rais Iajuddin Ahmed.Tangu wakati huo hadi watu 44 wameuawa na mamia wamejeruhiwa katika mapambano yaliyozuka kati ya makundi ya kisiasa yanayohasimiana.