1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Wakulima wachoma moto ofisi nchini Bangladesh

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlr

Wakulima zaidi ya 3,000 nchini Bangladesh jana walifanya mgomo na kuchoma ofisi ya serikali katika wilaya ya Chapainawabganj kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Machafuko hayo yalisababishwa na hatua ya maafisa wa serikali kutangaza mgao wa mbolea. Mkuu wa tarafa ya Nachal, Manjur Morshed, alijeruhiwa vibaya wakati wakulima walipoichoma moto ofisi yake.

Wakulima waliivamia ofisi hiyo wakati walipoambiwa wakulima wenye mashamba ya ekari moja wakatapewa gunia moja la mboloe na wengine watalazimika kugawana gunia moja miongoni mwao kwa sababu ya uhaba wa mbolea. Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika eneo hilo kuzima machafuko hayo.