1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Waziri mkuu wa zamani wa Bangladesh akamatwa

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBT4

Polisi nchini Bangladesh wamemtia mbaroni waziri mkuu wa zamani, Khaleda Zia, na mwanawe wa kiume kwa madai kwamba walihusika katika vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Walioshuhudia wanasema maafisa wa polisi waliwakamata washukiwa hao wakati walipokuwa nyumbani mwao mjini Dhaka saa chache baada ya kesi dhidi yao kuwasilishwa mahakamani na maafisa wa tume ya kupambana na rushwa nchini Nepal. Washukiwa hao baadaye walipelekwa kwenye mahakama moja mjini Dhaka.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni pamoja na kutoa kandarasi za kusimamia vituo viwili vya makasha makubwa ya vyuma ya kusafirishia mizigo wakati wa awamu ya mwisho ya Khaleda Zia kama waziri mkuu wa Bangladesh, iliyomalizika mwezi Oktoba mwaka jana.

Serikali ya sasa iliyo na idadi kubwa ya wanajeshi ilianzisha kampeni ya kupambana na rushwa wakati ilipoingia madarakani mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Waziri mkuu mwingine wa zamani wa Bangladesh, Sheikh Hasina, amekuwa akizuiliwa tangu alipokamatwa kwa madai ya kuhusika na rushwa miezi miwili iliyopita.