1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA.Ajali ya moto yauwa watu wawili

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOI

Takriban watu wawili wameuwawa kufuatia moto mkubwa uliozuka katika jumba moja refu mjini Dhaka nchini Bangladesh.

Inaaminika kuwa zaidi ya watu 90 wamekwama ndani ya jumba hilo.

Wazima moto wakisaidiwa na ndege za kikosi cha anga cha Bangladesh wamepambana kwa zaidi ya masaa sita kuuzima moto huo, watu wengine kadhaa waliokolewa baada kukimbilia juu kabisa ya jumba hilo.

Vituo viwili vya televisheni na ofisi moja ya magazeti vimo katika jumba hilo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.