1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA.´Maandamano ya kudai mageuzi yaingia siku yake ya pili

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt7

Maandamano ya upinzani kudai mageuzi katika utaratibu wa uchaguzi nchini Bangladesh yamechipuka upya mitaani huku mgomo wa kitaifa ukiingia siku yake ya pili na kuzorotesha shughuli zote za kawaida nchini humo.

Maelfu ya waandamanaji walijikusanya katika barabara kuu za mji wa Dhaka kulalamika juu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea kuhusu uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Januari mwakani.

Serikali ya mpito ya rais Lajuddin Ahmed imetishia kutuma wanajeshi ikihitajika ili kudumisha amani na utulivu.

Jana mtu mmoja aliuwawa na wengine kadhaa wakajeruhiwa baada ya waandamanaji walipoiwasha moto treni moja na kuwashambulia wafanyakazi wa shughuli za uchukuzi waliokataa kugoma.

Muungano wa vyama kumi na nne vya upinzani umeandaa mgomo huo kuhakikisha uchaguzi wa Januari unakuwa huru na wa haki.