1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Awamu ya pili ya uchaguzi nchini Timor Mashariki huenda ikafanyika

10 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAx

Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi uchaguzi nchini Timor Mashariki kuna dalili za kufanyika awamu ya pili ya uchaguzi nchini humo.

Huku chama tawala cha Fretilin kikijigamba kwamba kingeweza kushinda uchaguzi huo bila upinzani mkubwa, matokeo yanadhihirisha wagombea wa upinzani wakiendelea kupata kura zaidi. Matokeo hayo huenda yakalazimisha awamu ya pili ya uchaguzi ifanywe.

Francisco Lu Olo Guterres wa chama cha Fretilin, waziri mkuu Jose Ramos Horta, na kiongozi wa chama cha Democratic, Fernando Lasama De Araujo, wanaongoza mbele ya wagombea wengine watano wanaopigania urais wa Timor Mashariki.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amefurahishwa na jinsi uchaguzi wa Timor Mashariki ulivyofanyika kwa amani na utulivu.

Muangalizi mkuu wa uchaguzi huo, David Tollner, kutoka Australia pia ameridhika kwamba machafuko ya kikabila ambayo yameikabili Timor Mashariki, yalizuiliwa.