1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Jose Ramos-Horta aelekea kushinda uchaguzi wa urais Timor Mashariki

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3Z

Mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel, Jose Ramos-Horta anaelekea kushinda uchaguzi wa kwanza wa urais katika Timor Mashariki.

Ingawa shughuli ya kuhesabu kura inaendelea, kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi, Jose Ramos-Horta anatarajiwa kushinda uchaguzi huo kwa kishindo.

Tume ya uchaguzi imetoa matokeo ya awali yalioonyesha Jose Ramos-Horta ameshinda asilimia sabini ya kura kati ya asilimia tisini ya kura zilizohesabiwa.

Uchaguzi huo umelengwa kumchagua mtu atakayechukua mahali pa Rais Xanana Gusmao.

Uchaguzi huo ni wa kwanza nchini Timor Mashariki tangu mwaka 2002 miaka mitatu baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Indonesia.