1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Timor Mashariki yaelekea awamu ya pili ya uchaguzi

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAr

Matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Timor Mashariki yanatarajiwa kutangazwa hii leo. Maofisa wa uchaguzi tayari wameonya kwamba nchi hiyo inaelekea katika awamu ya pili ya uchaguzi na kuyumbayumba kwa hali ya kisiasa.

Waangalizi wa kimataifa wamesema huku asilimia 80 ya kura zikiwa zimehesabiwa, mgombea wa chama cha Fretilin, Francisco Ole Guterres anaongoza kwa asilimia 23.8 ya kura akifuatiwa katika nafasi ya pili na mshindi wa tunzo la amani la Nobel, Jose Ramos Horta, akiwa na asilimia 18.5.

Kiongozi wa upinzani, Fernando Lasama de Araujo, anashikilia nafasi ya tatu akiwa na asilimia 15.9 ya kura.

Ikiwa matokeo hayo yatathibitisha na tume ya uchaguzi, awamu ya pili ya uchaguzi itafanyika mnamo tarehe 8 mwezi ujao kati ya wagombea wawili wenye kura nyingi.