1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dili: Uchaguzi wa bunge waanza Timor Mashariki

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnC

Vituo vya kupiga kura vimefungulia kote katika Timor Mashariki kwa uchaguzi wa pili wa bunge tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 2002.

Chama tawala cha Fretilin kinakabiliana na chama cha National Congress of East Timor´s Reconstruction kilichoasisiwa na rais wa zamani, Xanana Gusmao.

Hakuna chama chochote kati ya vyama hivyo viwili kinachotarajiwa kupata ushindi wa moja kwa moja wa viti sitini na vitano vya bunge vinavyohitajika, hali hiyo ikiwa na maana kwamba chama kitakachoshinda kitalazimika kuunda serikali ya mseto pamoja na vyama vingine kumi na viwili vinavyoshiriki uchaguzi huo.