1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dini na siasa Ikulu Marekani

12 Septemba 2007

Marekani inateganisha dini na siasa.hatahivyo baada ya kuchaguliwa George Bush 2000,alimteua mjumbe maalumu kushughulikia maswali ya kanisa.

https://p.dw.com/p/CH8F

Rais George Bush anafahamika kuwa ndie rais mwenye itikadi kubwa ya dini kati ya marais wote walioingia Ikulu-White House-Marekani katika historia ya leo yanchi hii.Na hii licha ya kutenganishwa rasmi dini na serikali.

Sio tu rais George Bush katika baadhi ya maamuzi yake ya kisiasa ya kutatanisha huegemea hoja za itikadi ya dini yake,hata katika mashule mafunzo ya Darwin juu ya kuumbwa kwa mwanadamu kunatiliwa shaka.Wahafidhina wanaoegemea mafunzo ya dini nchini Marekani wanapinga ndoa za mashoga na misaada ya maendeleo ya Marekani, hutolewa zaidi kwa zile nchi zinazokataza mtindo wa kuharibu mamba.

Lakini, kufufuka kwa maadili ya kidini nchini Marekani, sio kuwa dola sasa linaongozwa chini ya misingi ya kidini na kwamba wimbi la waevanjelisti sasa limezuwiwa kusonga mbele.

Kwani wimbi hilo halitatia tena for a katika kampeni za uchaguzi wa rais wa hapo mwakani 2008 kinyume na vile lilivyoshawishi uchaguzi uliomleta madarakani George Bush.

Marekani kimsingi ndio nchi inayoabudu mno dini miongoni mwa zile zote za kiviwanda ulimwenguni.Kiasi cha thuluthi-mbili ya wamarekani wote,wanaenda makanisani na jumapili makanisa yanasheheni.Sehemu kubwa ya wamarekani wanaamini kuna maisha baada ya kifo.Je ni ajabu hapo kuwa dini ina ushawishi mkubwa hata katika siasa ?

Dini ina ushawishi wake katika siasa za dola hili,licha ya kuwa kutenganisha serikali na dini kumehifadhiwa kikatiba na hata rais George Bush, hawezi kubadili kitu hapo.

Alan wolfe,mtaalamu wa taftishi za mambo ya dini asema:

“Kutenganisha dini na kanisa Marekani, bado kumebakia pale pale hakujaguswa.Hii ni kwa sababu, dini inafaidika na sio kinyume chake.Barani Ulaya, kuna dola zinazofuata dini na zimo kufariki.

Marekani ambako uhuru wa dini umefaulu kutenganisha dola na dini,dini zinastawi.Laiti baadhi ya dini zingefaulu humu nchini kuondoa mfumo wa kutenganisha dini na serikali,basi hii ingepelekea kutoweka kwa dini nchini Marekani.”

Hatahivyo, Marekani chini ya utawala wa rais George Bush,dini imepiga hodi na kuingia ikulu-White House.

Hata kabla George Bush hakunadi vita vyake dhidi ya mihimili ya maovu ‘AXIS OF EVIL” duniani,jazba ya dini ilianza kuchemka.Hatua ya kwanza aliochukua Bush baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi wa kutatanisha wa 2000,alimteua mjumbe maalumu kuingia ikulu kushughulikia maswali ya kidini.Bush akitaka kuitua dola na jukumu lake ililobeba la kuwahudumia wanyonge katika jamii na kulitwika kanisa jukumu hilo.

Hii ilifanikiwa kiasi Fulani tu –anassema William Galston wa taasisi ya Brookings.

“Nadhani,uwezo wa kanisa haukukadiriwa vilivyo.Wengi wanahisi matokeo hasa ya jaribio hili ,hayakuwa makubwa.kama ilivyo sana katika siasa ,yapasa kutenganisha porojo na ukweli wa mambo.”