1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dominique Strauss-Kahn aachiliwa huru kwa mashtaka ya ngono

24 Agosti 2011

Hakimu mjini New York, Marekani, aliyatupilia mbali mashtaka ya ngono yaliomkabili mkuu wa zamani wa IMF, Dominique Strauss-Khan, hivyo kulimalizika lile sakata la udhalilishaji lilioharibu sifa ya mtu huyo.

https://p.dw.com/p/12Mnf
Dominique Strauss-Kahn na wakili wake wakiwa mahakamaniPicha: dapd

Jaji Michael Obus alilikubali ombi la mwendeshaji mashtaka la kuachana na kesi hiyo ambayo wameiona haiwezekani kushinda kutokana na mshtaki- mtumishi wa hoteli, Nafissatou Diallo, aliyemtuhumu Strauss-Kahn kufanya nae ngono kwa nguvu- kuwa alisema uwongo mara kadhaa, hivyo haaminiki. Strauss-Kahn, akitoka mahakamani na mkewe, Anne Sinclair, ambaye katika wakati wote tangu kashfa hiyo kujulikana, amemtea mumewe na kusema hana hatia, alisema amepumua na kumshukuru mkewe, watoto wake na kila mtu aliyemuunga mkono. Punde hivi Othman Miraji alizungumza na mwandishi wa habari wa mjini Paris, Mohammed Saleh, juu ya vipi wafaransa walivopokea habari za kuachiliwa huru Dominique Strauss-Kahn...

Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Mohamed Abdulrahman