1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmun na Bayern kukwaruzana

9 Aprili 2012

Joto la kinyang'anyiro cha kuwania taji la ligi kuu ya soka Ujerumani Bundesliga litaongezeka wakati Borussia Dortmund itakapoialika Bayern Munich siku ya Jumatano katika mpambano unaosubiriwa zaidi msimu huu.

https://p.dw.com/p/14ZoE
Fußball Bundesliga 13. Spieltag: FC Bayern München - Borussia Dortmund am Samstag (19.11.2011) in der Allianz Arena in München. Münchens Arjen Robben (l) und Dortmunds Marcel Schmelzer kämpfen um den Ball. Foto: Sven Hoppe dpa/lby (Achtung Sperrfrist! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung der Bilder im IPTV, Mobilfunk und durch sonstige neue Technologien erst zwei Stunden nach Spielende. Die Publikation und Weiterverwertung im Internet ist während des Spiels auf insgesamt fünfzehn Bilder pro Spiel begrenzt.) +++(c) dpa - Bildfunk+++
FC Bayern München - Borussia Dortmund Robben SchmelzerPicha: picture-alliance/dpa

Mabingwa watetezi Dortmund wana faida ya pointi tatu mbele ya mahasimu hao huku kukiwa na mechi tano zilizosalia. Bayern hata hivyo, wana faida kubwa ya mabao na huenda wakachukua usukani wa ligi mbele ya mashabiki 80,000 wengi wao wakiwa wapinzani. Dortmund haijashindwa katika mechi 23 mfululizo na waliishinda Wolsfburg magoli matatu kwa moja mwishoni mwa juma. Nao Bayern walisajili ushindi wa magoli mawili kwa moja nyumbani dhidi ya Augsburg.

Dortmund iliwazaba Bayern mara mbili kabla ya kutwaa taji la mwaka wa 2011 na tena nyumbani kwa Munich mapema msimu huu. Klopp anasisitiza kuwa kutakuwa na mechi nne zitakazosalia na hivyo Jumatano haitaamua mshindi wa taji.

Wengi wanatarajia kuona uhondo wa soka kutoka kwa wachezaji kama vile Shinji Kagawa, Ilkay Guendogan, Robert Lewandowski (Dortmund), Arjen Robben, Franck Ribery, Toni Kroos na mfungaji wa magoli mengi katika Bundesliga Mario Gomez (Munich).

Borussia Dortmund, mabingwa watetezi wa Bundesliga
Borussia Dortmund, mabingwa watetezi wa BundesligaPicha: dapd

Katika mechi nyingine zitakazochezwa katikati ya wiki, za Bundesliga, siku ya Jumanne Werder Bremen itakabana koo na Borussia Moenchengladbach. Hertha Berlin itacheza na Freiburg, Cologne itakuwa nyumbani kwa Mainz nao Augsbrug wakiwaalika VfB Stuttgart. Kisha siku ya Jumatano, Hanover na Wolfsburg watakutana, huku Bayer Leverkusen wakicheza na Kaiserslautern. Hamburg watakuwa kwa Hoffenheim nao Schalke wakifunga kazi dhidi ya Nuremberg.

Man United yaongeza pengo kileleni

Katika soka nchini Uingereza klabu ya Mnachester United inaonekana tayari kutwaa taji taji la 20 la Premier League baada ya kusajili ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya QPR na kuwaweka kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi nane mbele ya mahasimu wao wa karibu Manchester City ambao walishindwa na Arsenal goli moja bila jawabu.

Mkufunzi wa Man United Sir Alex Ferguson amemsifia Paul Scholes mwenye umri wa miaka 37 ambaye aligunga bao la pili katika mechi hiyo, ambalo ni la tatu tangu aliporejea tena kuiokoa Man United wakati alikuwa amestaafu mwezi Januari. Ferguson anasema Scholes ndio sababu muhimu ya kuibuka kwa United ambao wameshinda mechi 11 mfululizo kati ya 12 za ligi ya premier.

Manchester City iliongoza ligi kwa kipindi kirefu kabla ya kuzembea
Manchester City iliongoza ligi kwa kipindi kirefu kabla ya kuzembeaPicha: dapd/DW-Montage

Katika habari nyingine ni kuwa hatima ya mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli inaning'inia kwenye mizani baada ya mkufunzi Roberto Mancini kukiri kuwa subira yake na mchezaji huyo imeanza kuisha. Balotelli alitimuliwa uwanjani kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwa mara ya tatu msimu huu, katika dakika ya 89 wakati matumaini ya City kunyakua taji la ligi yalipozikwa na Arsenal.

Huenda FA ikachukua hatua

Mancini ambaye kila mara amekuwa akimuunga mkono Balotelli, jana alisisitiza baada ya mchuano wa jana kuwa Muitalia huyo ni lazima aibadili mienendo yake, akisema huenda akauzwa ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Mancini alisema Balotelli hatocheza tena katika mechi sita zilizosalia msimu ukikamilika. Shirikisho la soka Uingereza FA linatarajiwa kumchukulia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hatua kali za kinidhamu.

Kule Uhispania, Real Madrid walitoka sare ya bila kufungana na Valencia mwishoni mwa juma na hivyo kupunguza pengo baina yao na nambari mbili Barcelona hadi tofauti ya pointi nne. Real sasa watakutana na mahasimu wao Atletico Madrid siku ya Jumatano. Barcelona nao watakuwa uwanjani nyumbani Jumanne dhidi ya Getafe.

Mwandishi/Mtayarishaji: Bruce Amani/AP/Reuters/DPA

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman