1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yaendeleza rekodi ya ushindi

30 Aprili 2012

Mabingwa wa Ligi ya Soka Ujerumani Bundesliga Borussia Dortmund walikaribia kuandikisha rekodi nyingine baada ya kuwazaba Kaiserslauten walioshushwa daraja magoli 5 - 2, ikiwa ni ushindi wa 27 mfululizo.

https://p.dw.com/p/14nFP
Rheinland-Pfalz/ Fussball, 1. Bundesliga, Saison 2011/2012, 33. Spieltag, 1. FC Kaiserslautern - Borussia Dortmund, Samstag (28.04.12), Fritz-Walter-Stadion, Kaiserslautern: Dortmunds Lucas Barrios (l.) und Kaiserslauterns Mathias Abel kaempfen um den Ball. +++ Achtung Bildredaktionen: Die Verwendung der Bilder fuer die gedruckten Ausgaben der Zeitungen und andere Print-Medien ist ohne Einschraenkungen moeglich. Die DFL erlaubt ausserdem die Publikation und Weiterverwertung von maximal sechs Bildern pro Spiel im Internet. Eine Weiterverwertung im IPTV, Mobilfunk und durch sonstige neue Technologien ist erst 2 Stunden nach Spielende der jeweiligen Wettbewerbsspiele der Bundesliga und 2. Bundesliga erlaubt! Foto: Thomas Wieck/dapd
Fussball 1. Bundesliga 1. FC Kaiserslautern gegen Borussia DortmundPicha: dapd

Baada ya kuvunja rekodi ya Bundesliga kwa kushinda mechi nyingi mfululizo katika msimu mmoja, Dortmund sasa wako rekodi moja tu nyuma ya ile ya Bayern Munich ya pointi 79 zilizokusanywa katika msimu mmoja wa Bundesliga, ambayo walipata mara mbili katika miaka ya 70. Bayern nao walishinda Stuttgart magoli mawili kwa sifuri.

Mfungaji wa magoli mengi katika Bundesliga Klaas-Jan Huntelaar alifunga magoli mawili na kuhakikisha kuwa Schalke inafuzu katika ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya klabu hiyo kuwazaba Hertha Berlin mabao manne kwa sifuri Jumamosi. Lewis Holtby na Raul Gonzalez ambaye alicheza mchuano wake wa mwisho pia walifunga mabao. Ushindi wa Freiburg wa magoli manne kwa moja dhidi ya Cologne uliiokoa Hertha kutoshushwa ngazi angalau kwa sasa. Hertha iko pointi mbili nyuma ya Cologne katika eneo la michuano ya kuamua atakaefurushwa katika ligi wikendi ijayo.

Schalke 04 wamerejea tena katika kinyang'anyiro cha Ulaya
Schalke 04 wamerejea tena katika kinyang'anyiro cha UlayaPicha: picture-alliance/dpa

Augsburg na Hamburger SV wako salama baada ya kutoka sare za bila kufungana dhidi ya Borussia Moenchengladbach na Mainz. Wolfsburg iliimarisha matumaini yao ya kucheza katika Ligi ya Ulaya baada ya kuilaza Werder Bremen magoli matatu wka moja, nayo Nuremberg ikaishinda Hoffenheim matatu kwa mawili.

Podolski ahamia Arsenal
Uhamisho wa mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Ujerumani Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne kuelekea Arsenal umekamilishwa. Klabu hiyo ya ligi ya Bundesliga imesema kuwa Podoslki atajiunga na Arsenal ya Uingereza kuanzia msimu ujao kwa kiasi cha pesa ambacho hakikutangazwa.

Uvumi kuhusu uhamisho wa Lukas Podolski umekuwa ukienea
Uvumi kuhusu uhamisho wa Lukas Podolski umekuwa ukieneaPicha: dapd

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Cologne akiwa na umri wa miaka 10 na ataungana na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ujerumani Per Mertesacker katika klabu hiyo ya Premier League.

Mchezaji raia wa Peru Jefferson Farfan atasalia katika klabu ya Schalke 04. klabu hiyo imesema Farfan amekubali kuurefusha mkataba wake kwa miaka mine hadi mwisho wa mwezi Juni mwaka 2016. Farfan amefunga magoli 24 katika mechi 114 za ligi alizocheza tangu alipojiunga na Schalke akitokea PSV Eindhoven mnamo mwaka a 2008.

Kagawa kuondoka Dortmund?
Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund wanatarajiwa kumpoteza nyota wao Shinji Kagawa, ambaye anasemekana kuzingatia kujiunga na Ligi ya Uingereza. Kuna uvumi kuwa analenga kuhamia Man United.

Shinji Kagawa amekuwa akisitasita kutia saini mkataba mpya na Borussia Dortmund
Shinji Kagawa amekuwa akisitasita kutia saini mkataba mpya na Borussia DortmundPicha: Reuters

Rais wa Dortmund Reinhard Rauball amemwambia kiungo Kagawa mwenye umri wa miaka 23 raia wa Japan ambaye mkataba wake unakamilika mwaka wa 2013, ni lazima atie saini y akuurefusha mkataba wake leo. Dortmund imekuwa ikifanya mazungumzo na wakala wa Kagawa kuhusu mktaba huo bila kufua dafu.

Na Klabu ya Uingereza Chelsea ilianza maandalizi ya msimu mpya baada ya makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati Mjerumani Marko Marin kutoka Werder Bremen. Chelsea ilisema Jumamosi kuwa imekubali kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na kwamba Marin amekubali kanuni zote za mkataba.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/Reuters/DPA
Mhariri: Moahammed Abdul-rahman