1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA: Sababu ya ajali ya ndege yachunguzwa

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3g

Wataalamu kutoka Kenya,Cameroon na Marekani wameanza kuchunguza sababu ya ajali ya ndege ya shirika la “Kenya Airways” iliyotokea Jumamosi iliyopita muda mfupi tu baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Douala nchini Cameroon.Watu wote 114 wamepoteza maisha yao katika ajali ya ndege hiyo aina ya Boeing 737-800.Siku ya Jumatano,mkuu wa shirika hilo la ndege,Titus Naikuni alisema, chombo cha kunasia sauti cha ndege hiyo,bado hakijapatikana.Na mwenyekiti wa “Kenya Airways” Evanson Mwaniki amesema,shirika hilo la ndege linatuma Cameroon,wapelelezi maalum wa Kingereza kusaidia kutambulisha maiti zinazokusanywa.