1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru

Admin.WagnerD30 Juni 2015

Upinzani Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo umesema rais Joseph Kabila hajaonyesha nia ya wazi ya kuweko na uchaguzi mkuu nchini humo.

https://p.dw.com/p/1Fq0h
Joseph Kabila Kabange
Rais Joseph KabilaPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Rais Kabila ambae amelihutubia taifa katika madhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Kongo leo , amesema kwamba uchaguzi ujao utakuwa wa utulivu na amani , huku akiwaomba wapinzani kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili kujadili changa moto za uchaguzi.Hata hivyo Kabila ambaye hakutaja ikiwa atagombea au la, ametupilia mbali pendekezo la kuweko na msuluhishi wa kimataifa katika mazungumzo hayo kama wanavyodai wapinzani.
Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.

Mwandishi Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman