1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Mwanamuziki Pepe Ndombe Opetum afariki dunia

25 Mei 2012

Mwanamuziki mashuhuri wa bendi ya BANA OK, amefariki hapa mjini Kinshasa kufuatia maradhi ya masaa kadhaa.

https://p.dw.com/p/152T6
Wanamuziki wa Kongo wampoteza mwenzao Pepe Ndombe Opetum
Wanamuziki wa Kongo wampoteza mwenzao Pepe Ndombe OpetumPicha: Mark Johnson

PEPE NDOMBE OPETUM naibu kiongozi wa bendi ya Bana Ok amekufa akiwa na umri wa miaka 68. Alipata umaarufu wakati alipokuwa akiimba na Hayati Luwambo Makiadi na Lutumba Simaro . Wimbo wake wa MOKOLO NA KOFUFA (Siku nitakayo fariki) ndio maarufu sana katika eneo la Afrika Mashariki na Kati na uliompandisha kwenye jukwaa la waimbaji bora wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa anaarifu zaidi juu ya kifo cha Pepe Ndombe

(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni)

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Saleh Mwanamilongo