1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dresden:Wana CDU wataka ada ya shule za chekechea ifutwe kusaidia familia

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoc

Katika mkutano wao wa mwaka mjini Dresden, wanachama wa chama cha Christian Demokratik-CDU, cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, wameitaka serikali izisaidie familia kwa kufuta ada ya shule za chekechea-kindergarten mwaka ujao.Ujerumani inakabiliwa na tatizo la kupungua idadi ya wakaazi, kukiwa na watoto wachache na wingi wa wazee.Wajumbe pia walitoa wito wa mtihani wa lugha kwa watoto wa miaka mine, wakiwemo wahamiaji, kuhakikisha wanajifunza Kijerumani. Akihutubia mkutano wa chama cha CDU, Waziri mkuu wa mkoa wa Bavaria Edmond Stoiber ambaye pia ni Kiongozi wa chama ndugu cha CSU, alikilaumu chama cha Social demokratik SPD, washirika wa Merkel katika serikali ya muungano, kwa kuzuwia juhudi za kuwa na vyombo zaidi vya video vya ukaguzi , pamoja na sheria kuhusu wageni. Mkutano huo wa chama cha CDU unamalizika leo.