1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DR.RICE ASWAN

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFj

WASHUJNGTON:

Waziri wa nje wa Marekani Dr.Condoleeza Rice yuko njiani kwa safari ya Mashariki ya Kati kwa mazungumzo yenye shabaha ya kufufua utaratibu wa amani uliozorota baina ya Israel na wapalestina.

Dr.Rice atakutana na viongozi wa Jordan,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za kiarabu-Emirates na Misri huko Aswan,Misri.Hii itakua ziara yake ya kwanza huko tangu kuundwa kwa serikali mpya ya wapalestina ya umoja wa taifa inayojumuisha wanachama wa Hamas wenye siasa kali na wale wa Fatah wa siasa ya wastani.

Na Taarifa kutoka RAMALLAH zinasema ,waziri mpya wa mambo ya nje wa Palestina Ziad Abu Amr atazuru Ufaransa karibuni-ikiwa ziara yake ya kwanza tangu kuundwa kwa serikali hiyo ya Umoja wa taifa wiki iliopita.