1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI : Kimbunga kikali chaelekea Muscat

6 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuT

Kimbunga kikali ambacho kimepiga mwambao wa mashariki wa Oman na kulazimisha serikali kuwahamisha maelfu ya watu kutoka maeneo ya tambarare hivi sasa kinaelekea kwa haraka mjini Muscat.

Hali ya hatari imetangazwa nchini humo.Polisi na jeshi wamewekwa kwenye hali ya tahadhari mbali na kuwekwa kwa vikosi vya kushughulikia hali ya dharura na vile vya ulinzi vya raia kukabiliana na hali ya dharura kutokana na kimbunga hicho kama vile mafuriko.

Ahmed Al Harthy Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa amesema kimbunga hicho kinaelekea Muscat pembezoni mwa mwambao na kwamba wanataraji kuwa kitapiga Muscat saa kumi jioni.

Iran leo hii pia imewahamisha mamia ya wakaazi wa mji wa bandari wa Chabahr ulioko kwenye mwambao wa bahari ya Oman kwa kuhofia kimbunga hicho.