1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI : Wanamgambo waionya tena Ujerumani

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK7

Kundi linaloaminiwa kuwa na mafungamano na kundi la Qaeda limeionya Ujerumani na Austria kwamba zitakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo venginevyo zinaondowa wanajeshi wao kutoka Afghanistan.

Onyo hilo limetolewa kwenye ukanda mpya wa video uliowekwa katika mtandao na linafuatia tangazo lililowekwa hapo jana na kurushwa na vituo vya televisheni vya Kiarabu ambapo kwayo wanamgambo wa Iraq wameonekana wakimshikilia mateka mwanamke wa Kijerumani na mwanawe wa kiume na kutishia kuuwauwa venginevyo Ujerumani inaviondowa vikosi vyake kutoka Afghanistan katika kipindi kisichozidi siku 10.

Ujerumani ina takriban wanajeshi 3,000 wanaotumikia kikosi cha Usaidizi wa Usalama cha Kimataifa kinachoongozwa na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO nchini Afghanistan wakati Austria ina maafisa watano wa kijeshi nchini humo.