1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI:Al Qaida yasikitika mpango wa kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Irak utawanyima nafasi ya kuwaangamiza

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4S

Msaidizi wa Kiongozi wa Al Qaida Ayman al Zawahri amesema kuwa muswaada uliyoidhinishwa na bunge la congress la Marekani kutaka kuondoshwa kwa majeshi yake nchini Irak, ni uthibitisho wa kushindwa kwa Marekani.

Akizungumza katika mkanda wa video, al Zawahri amesema kuwa muswaada huo unaonesha kushindwa na kuchangayikiwa kwa wamarekani.

Lakini hata hivyo amesema kuwa muswaada huo, utawanyima nafasi ya kuyaangamiza majeshi ya Marekani ambayo amesema kuwa wameyaweka katika mtego wa kihistoria.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani alikataa kuzungumzia lolote juu ya mkanda huo wa video ambao umetoka siku nne tu baada ya Rais Bush kutumia kura ya turufu kuidhinishiwa fedha za ziada kwa ajili ya jeshi lake huko Irak lakini kwa sharti la kuanza kuondoka Oktoba mosi mwaka huu.