1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI:Benazir Bhutto athibitisha kurudi nyumbani Alhamisi

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7F3

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto anathibitisha kuwa anarejea nchini mwake hapo kesho ili kushiriki katika kampeni za uchaguzi unaopangwa kufanyika mwaka ujao.Mwanasiasa huyo wa chama kikubwa cha upinzani cha Pakistan Peoples Party ,PPP alienda uhamishoni zaidi ya miaka minane iliyopita alipokabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Kiongozi huyo wa upinzani anakataa kutimiza maombi ya Rais Jenerali Pervez Musharraf ya kuahirisha safari yake hadi baadaye.Aidha Bi Bhutto anakabiliwa na vitisho vya kuuawa na wapiganaji wa Pakistan wa Taleban.Kulingana na duru za kuaminika Bi Bhutto huenda akafikia makubaliano ya kugawana madaraka na Jenerali Pervez Musharraf.