1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI:Bibi Bhutto asema huenda akarejea Pakistan

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZz

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan bibi Benazir Bhutto amesema kwambá anatarajia kurejea nchini Pakistan katikati ya mwezi Oktoba ili kushiriki katika uchaguzi na pia huenda akajiunga na jenerali Parves Musharraf kwa sharti kwamba rais Musharraf ataondosha kikwazo kinachowapinga mawaziri wakuu kugombea awamu ya tatu ya uongozi.

Hata hivyo habari kutoka nchini Pakistan zinasema kwamba rais Pervez Musharraf amewataka mawaziri wakuu wa zamani bibi Benazir Bhutto na bwana Nawaz Sharif wajiweke kando hadi uchaguzi ujao utakapomalizika.

Bibi Benazir Bhutto aliyeripotiwa kukutana na rais Parvez Musharraf mwezi uliopita amesisitiza juu ya msimamo wake wa kumtaka rais Musharraf aachie ngazi za kijeshi.