1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI:Marekani yakanusha meli yake kushambuliwa

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEu

Jeshi la Marekani limekanusha taarifa kuwa Iran imeishambulia kwa makombora meli yake ya kivita huko Ghuba.

Kamanda wa kikosi cha tano cha jeshi la majini la Marekani huko Ghuba, Charles Brown amesema kuwa meli zote za kivita za Marekani katika eneo hilo ziko salama baada ya kufanyiwa uchunguzi na kwamba habari hizo ni uzushi.

Uvumi ya kwamba Iran imefanya shambulizi hilo, umepelekea kupanda ghafla kwa bei ya mafuta kwa asilimia 8 ambapo pipa moja limefikia kiasi cha dola 68.