1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBLIN: Ireland Kaskazini yapiga kura kuhusu kikosi cha polisi.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX3

Wafuasi wa chama kikuu cha kikatoliki cha Ireland Kaskazini wamekusanyika mjini Dublin kupiga kura ya kukubali au kukataa kikosi cha polisi katika eneo hilo linalotawaliwa na Uingereza.

Suala la chama cha Sinn Fein kuunga mkono kikosi hicho cha polisi limekuwa kizingiti kikubwa cha jaribio la kupatikana serikali inayogawana madaraka kati ya Wakatoliki na Waprotestanti.

Chama cha Sinn Fein, kilikuwa tawi la kisiasa la kundi la waasi la Irish Republican Army na kiliunga mkono juhudi za kundi hilo kupindua kwa mabavu utawala wa Ireland Kaskazini.