1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUISBURG : Wataliana sita wauwawa Ujerumani

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYm

Wanaume sita wa Italia wameuwawa kwa kupigwa risasi karibu na kituo cha reli katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Duisburg shambulio ambalo inarepotiwa kuwa yumkini likawa lanahusiana na mfarakano wa kihalifu.

Maiti tano zilipatikana kwenye magari mawili nje ya mkahawa mmoja wa Kitaliana wakati mtu wa sita alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.Msemaji wa polisi ya Ujerumani amesema wahanga hao wenye umri kati ya miaka 16 na 39 wote wamepigwa risasi kichwani.Polisi imesema kwamba watu hao sita walikuwa wana husika na ukoo ulioko kwenye mfarakano wa mauaji wa muda mrefu katika mkoa wa Calabria nchini Italia.

Mzozo huo unajuliana kama mfarakano wa San Luca uliopewa jina la kijiji husika ulianza mwaka 1971.