1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya 13 ya mazungumzo kati ya Ujerumani na Urusi

19 Julai 2011

Kansela Angela Merkel amekutana na rais wa Urusi Dmitri Medvedev mjini Hannover katika mkutano wa kilele uliogubikwa zaidi na masuala ya nishati.

https://p.dw.com/p/11zbh
Kansela Angela Merkel (kulia) na rais Dmitri Medvedev wanakwenda kuweka shada la mauwa katika kiunga cha makaburi ya wenye kuheshimiwa huko HannoverPicha: dapd

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mgeni wake wa kutoka Urusi Dmitri Medvedev walishiriki kwanza katika kikao kinachojulikana kama "Mdahalo wa Petersburg"-mdahalo unaoendelea tangu miaka 11 sasa na kuwaleta pamoja wawakilishi wa mashirika ya jamii kutoka nchi hizi mbili.

"Katika demokrasia watu wanapendelea zaidi kuzungumzia yale yasiyoendelea vizuri ,badala ya yanayoendelea vizuri-"amesema kansrla Angela Merkel.

"Afadhali kuvutana mara moja kuliko kukaa kimya" aliongezea rais wa Urusi Dmitri Medvedev.

Rais Medvedev na kansela Angela Merkel anaezungumza kwa fasaha kirusi hawajataka kugusia masuala tete mfano wa yale yanayohusiana na haki za binaadam.

Hata hivyo kansela Merkel amekiri yeye ndie sababu ya kukwama mazungumzo kati ya Urusi na Ulaya kuhusu kuachana na utaratibu wa kutolewa visa-mada ambayo ni muhimu sana kwa Moscow.

Deutsch-Russische Regierungskonsultationen 2011
Mkutano wa mawaziri wa Ujerumani na UrusiPicha: dapd

Kwa upande wa Ujerumani,mwenyekiti mwenza wa "Mdahalo wa Petersburg,waziri wa ulinzi Lothar de Maizière amesema Democratia ni muhimu katika kuigeuza Urusi iwe ya kimambo leo,akikumbusha tawala za kiimla mfano Umoja wa zamani wa Usovieti na Ujerumani ya zamani ya wanazi,hazikudumu.

Katika kikao hiki cha 13 cha mwaka kati ya serikali za Urusi na Ujerumani,nishati ndiyo iliyokuwa kitovu cha mazungumzo,Moscow ikiwa na hamu ya kuzidi kujijenga katika sekta hiyo.

Makubaliano kadhaa yametiwa saini wakati wa mkutano kati ya pande hizi mbili.Katika mkutano na waandishi habari mwishoni mwa mazungumzo yao,kansela Angela Merkel amesema:

"Idadi ya mikataba iliyotiwa saini ni ushahidi wa maingiliano ya dhati kati ya sekta tofauti na kati ya wizara tofauti-maingiliano yanayoendelezwa tangu miaka kadhaa iliyopita kati ya serikali ya Ujerumani na serikali ya Urusi."

Mikataba 12 imetiwa saini katika sekta ya kisiasa,kiuchumi na elimu ya juu.

Makampuni ya Ujerumani, amesema kansela yanashirikiana na Urusi.Wajasiria mali wa Ujerumani wanapendelea kuwekeza katika sekta tofauti za kiviwanda tangu vidogo vidodo mpaka vya wastani.

Urusi ingependelea kuimarisha vinu vyake vya nishati inayoptokana na gesi na kuzidisha kiwango cha gesi inayoletwa Ujerumani.

EU Putin Brüssel
Waziri mkuu wa Urusi Vladimir PutinPicha: dapd

Ziara ya rais Medvedev nchini Ujerumani imefanyika baada ya mvutano kuzuka nchini Ujerumani baada ya uamuzi wa kutunukiwa waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin tuzo ya Quadriga kubatilishwa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir,dpa/Reuters,afp

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed