1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais Serbia

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1aR

BELGRADE:

Leo katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais,wapiga kura nchini Serbia wanamchagua atakaeshika wadhifa huo katika nchi hiyo ya Balkan.Rais wa hivi sasa Boris Tadic na mpinzani Tomislav Nikolic wanatazamiwa kwenda bega kwa bega katika kinyanganyiro kitakachoamua njia itakayofuatwa na Serbia kuhusu Umoja wa Ulaya.

Tadic anehesabika kama kiongozi anaelemea kambi ya Magharibi akitaka kuiongoza Serbia kuwa mwanachama katika Umoja wa Ulaya.Kwa upande mwingine,mzalendo Tadic anataka ushirikiano wa karibu zaidi pamoja na Urusi.Mada mojawapo kuu katika uchaguzi wa rais nchini Serbia ni suala linalohusika na kujitenga kwa jimbo lake la kusini,Kosovo.Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zinaunga mkono uhuru wa Kosovo lakini Belgrade inapinga kabisa hatua ya aina hiyo.