1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru yya kwanza ya klabu bingwa Afrika

15 Februari 2008

Duru ya kwanza ya kombe la CAF na klabu bingwa yaanza na Blatter aionya Ligi ya uingereza.

https://p.dw.com/p/D8B5

Mbali na kurudi kinyan’ganyiro cha kombe la klabu bingwa na kombe la shirikisho la Afrika-Confederation cup uwanjani mwishoni mwa wiki hii,rais wa FIFA-Sepp Blatter ameikemea Premier League-Ligi ya Uingereza kwa mpango wake wa kutaka kucheza baadhi ya mechi zake za Ligi nchi za n’gambo na amesema FIFA haitakubali.

Mkataba wa Roger Lemere- mfaransa kocha wa Tunisia iliotolewa katika nusu-finali ya kombe la Afrika na simba wa nyika-kamerun hautarefushwa .Bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon-mkenya Paul Tergat amesema atakwepa kushiriki katika london marathon April ijayo kwavile ndio kwanza amerudi kwa mazowezi.

Wakati klabu kadhaa zimeingia uwanjani jana na leo kwa duru ya kwanza ya kombe la klabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho,sehemu kubwa yxa majogoo wa afrika waliocheza kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana wamerejea klabu zao barani Ulaya.

Miongoni mwao ni jogoo la Kamerun-Samuel Eto’o alieumia lakini katika finali ya jumapili iliopita kati ya mabingwa Misri na simba wa nyika-kamerun.

Samuel Eto’o alieibuka katika kombe la Afrika mtiaji mabao mengi kabisa (mabao 5) ameanza kufanyiwa haraka matibabu na klabu yake ya Barcelona ili awe fit kwa changamoto ya kati ya wiki hii ijayo na Celtic ya Scotland kuania champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Eto’o istishe, aliivunja ile rekodi ya mabao 14 katika kombe la Afrika iliowekwa na Muivory Coast Laurent Pokpou kwa mabao yake 16 katika kombe hili hadi sasa.

Si ajabu kwahivyo, kwanini FC Barcelona, inamhitaji arudi uwanjani na mapema.

Stadi mwengine ambae alitia fora katika kombe la Afrika nchini Ghana na anaesakwa na Manchester united ni muamngola MANUCHO.Ombi la Manchester la kumpatia ruhusa ya kufanya kazi nchini Uingereza mapema mwaka huu,lilikataliwa na wizara ya ndani kwa sababu Manucho hakuichezea bado timu ya Taifa ya Uingereza kwa kiasi cha mapambano yake 75 kati ya 100.

Manchester inapanga sasa kutoa ombi jipya katika majira ya kiangazi mwaka huu kwa wizara hiyo ya ndani ikitumai kuwa manucho ataichezea Manchester alao msimu ujao.

Alao makocha 2 waligonga vichwa vya habari baada ya kumalizika kwa kombe la Afrika:mmoja ni yule wa simba wa nyika-kamerun-mjerumani Otto Pfister na mwengine ni mfaransa –kocha wa Tunisia –Roger Lemere.Wakati Otto Pfister mwenye umri wa miaka 70 ametangaza kubakia na simba wa nyika-makamo bingwa wa Afrika hadi kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini.

Ama kuhusu Roger Lemere,yeye amepigwa shoka baada ya Tunisia kupigwa kumbo katika robo-finali ya kombe la Afrika nchini Ghana.Shirikisho la dimba la Tunisia FTF liliarifu juzi kwamba mkataba wa Roger Lemere unaodumu hadi mwishoni mwa mwezi juni,mwaka huu hautarefushwa.

Tunisia ilizabwa mabao 3-2 na Kamerun na vyombo vya habari vya tunisia vikahanikiza atimuliwe.

Lemere mwenye umri wa miaka 66 aliiongoza Ufaransa kutwaa kombe la Ulaya la mataifa mwaka 2000 na aliongoza Tunisia tangu mwaka 2002 na kutwaa kombe la Afrika nyumbani 2004.

Tunisia itaanza duru ya kwanza ya kuania tiketi ya kushiriki katika kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini na kombe la Afrika la mataifa mwaka huo nchini Angola hapo juni ikiwa na miadi na Burkina Faso,Burundi na Seyschelles katika kundi la 9.

Makamo-rais wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni-Jack Warner anasema hataiungamkono Uingereza kuandaa kombe la dunia 2018.Siku za nyuma Warner amekua akikosoa mchango wa uingereza katika dimba ulimwenguni na anadai kwamba England imesubiri kitambo sana hadi kujitokeza sasa kutaka kuandaa kombe hilo la dunia.Warner alisema August mwaka jana atafanya kila awezalo kuitia munda Uingereza isiandae Kombe la dunia ambalo kwa mara ya mwisho 1966.

Mwaka huo iliilaza Ujerumani mabao 4-2 na kuvaa taji.

Hatahivyo,Jack Warner alitumai timu ya taifa ya uingereza itacheza mechi ya kirafiki kwao nchini Trinidad na Tobago hapo juni mwaka huu ikiadhimisha mwaka wa 100-centenery wa chama chake cha mpira (FA).England na Trinidad na Tobago zilikumbana mara moja katika kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani na Uingereza ikashinda chupuchupu kwa mabao 2-0 huko Nüremberg.

Wakati makamo-rais wa FIFA anapinga Uingereza kuandaa kombe la dunia 2018, rais wa FIFA Sepp Blatter wiki hii alipinga wiki hii mradi wa Ligi ya Uingereza-premier League wa kucheza baadhi ya mashindano yake ya Ligi nje ya Uingereza.Blatter aliueleza mpango huo ni kutumia vibaya dimba la Uingereza.Akaionya nae Uingereza ikiendelea na mpango huo,basi kwa kadiri yeye ni rais wa FIFA,hataruhusu Uingereza kuandaa kombe la dunia kama itakavyo 2018.

Kisa hasa ni nini ?

Klabu 20 za Premier League-ligi ya Uingereza zimeafikiana kucheza mechi zao za Ligi msimu wa mwaka 2010 kwendea 2011 nchi za n’gambo chini ya pendekezo lililotolewa wiki iliopita.Rais wa FIFA alikanusha madai ya mkurugenzi wa Premier League-Peter Scudmore kuwa FIOFA haiweezi kuingilia kuzuwia mpango huo ikiwa klabu za england zimekubaliwa kusonga mbele na mradi huo na chama cha mpira cha Uingereza.

Nae rais wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya,mfaransa Michel Platini,ameuita mpango huo ni wa kuchekesha na kiroja cha mambo.

Ikijiandaa kwa kombe lijalo la Ulaya la mataifa nchini Uswisi na Austria, timu ya taifa ya Ujerumani ina miadi mwezi ujao na Uswisi kwa dimba la kirafiki.Kocha wa makipa wa ujerumani amemuonya kipa wa taifa Jens Lehmann kwamba atabidi kutamba kweli langoni kuhakikisha nafasi yake langoni.Lehmann si kipa nambari 1 katika lango la klabu yake ya Arsenal na tangu kuwa hivyo ,amekuwa aikitiliwa shaka iwapo ni yeye anaestahiki kulinda lango hilo.Licha ya kwamba Ujerumani iliikomea Austria mabao 3:0 hapo Februari 5,Lehmann alionesha dosari nyingi.Kwahivyo, kocha wa kipa wa taifa wa Ujerumani Koepke amemshauri Lehmann kutamba langoni siku hiyo au sivyo nafasi yake huenda ikachukuliwa na kipa mwengine.Koepke alitamani kuona Lehmann anapewa changamoto na kipa mwengine kama yeye alivyompa changamoto Oliver kahn hadi alipostaafu.

RIADHA:

Bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon-mkenya Paul Tergat amearifu kwamba hatashiriki katika london marathon mwezi wa April kwavile ndio kwanza ameanza mazowezi baada ya mafunzo ya miezi 4 ya kijeshi.Hivi sasa yupo fit kwa asili-mia 40 tu na mbio hizo zinakaribia.Kwahivyo, Tergat alisema macho yake yote atayakodoa katika mbio za Olimpik za Beijing.Wakati wa machafuko ya uchaguzi nchini kenya, Paul tergat amekuwa akihudhuria mafunzo huko Nakuru,mkoa wa rift Valley.

Michezo ya olimpik ya beijing ikiwa nusu mwaka kabla kuanza, imekuwa ikigonga vichwa vya habari visivyohusu michezo hiyo-siasa: Rais george Bush wa marekani lakini, hakusudii kucheza siasa na olimpik na hivyo amesisitiza kwamba atahudhuria michezo ya beijing licha ya ila zinazozidi kwa china na siasa yake nchini Sudan.

Rais Bush alisema kwamba, atakwenda beijing kwavile anaiangalia Olimpik ni tokeo la kispoti na si la kisiasa.

Mpigaji-filamu wa kimarekani Steven Spielberg mapema wiki hii alijitenga na michezo ya olimpik ya beijing kuwa mshauri wa tafrija za kisanaa za michezo hiyo.Aliituhumu China kutofanya vya kutosha kuishinikiza Sudan-mshirika wake kukomesha maafa ya Dafur,mkoa wake wa magharibi.