1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUSHANBE: Uchaguzi wa urais nchini Tajikistan haukuwa wa kidemokrasia halisi

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv3

Wachunguzi wa Ulaya waliosimamia uchaguzi wa urais nchini Tajikistan wamesema uchaguzi huo haukufikia kiwango cha kidemokrasia kinachostahili. Shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya, OSCE kwa ufupi, limesema ukosefu wa chaguo jingine bali na rais Emomali Rakhmonov umeshusha imani juu ya kura hiyo. Matatizo mengine yaliojitokeza ni pamoja na wapigaji kura kuwapigia kura jamaa zao na saini zimefanana huku na kule katika daftari za wapigaji kura.

Rais Rakhmonov ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais na asili mia 79 ya kura. Mpinzani wake, Olimzhon Boboyev, alipata chini ya asili mia 7 tu. Lakini vyama muhimu vya upinzani vilisusia uchaguzi huo.