1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW Inawaalika katika kongamano maalum tarehe 24 mwezi huu huko Dar es salaam

26 Februari 2010

Waandishi mbali mbali maarufu wa habari Tanzania watazungumza katika kongamano hilo ambao ni Jenerali Ulimwengu, Tido Mhando, Ananilea Nkya, Ayoub Rioba na Majjid Mjengwa.

https://p.dw.com/p/M5z6
Mhariri mkuu wa DW radio na Internet Marc Koch.Picha: Archiv

Idhaa ya DW pamoja na taasisi ya mafunzo ya lugha na Utamaduni wa kijerumani ya Goethe nchini Tanzania zinapenda kuwaalika nyote wasikilizaji katika ufunguzi rasmi wa kituo maalum cha kupata maelezo kuhusu matangazo ya DW kitakachokuwa ndani ya taasisi hiyo ya Goethe jijini Dar es salaam.

Ute Schaeffer
Mkuu wa matangazo ya idhaa za lugha za kiafrika na mashariki ya kati,Ute Schaeffer.Picha: DW

Sherehe hizo za Ufunguzi zitafanyika tarehe 24, saa sita mchana, katika Goethe Institut.Kituo hicho maalum cha ''DW Punkt'' kitakupa fursa wewe mwanafunzi na wageni wengine kuweza kujua mengi kuhusu DW, kupitia Televisheni,Radio na mtandao wa Internet moja kwa moja. Pia baada ya sherehe hizo za Ufunguzi, DW pamoja na taasisi ya DED/INWENT ingependa pia kuwaalika katika mjadala maalum, utakaozungumzia mchango wa vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu nchini Tanzania. 

Mjadala kuhusu Demokrasia Tanzania

DW Radio Logo
Nembo ya Deutsche Welle

Mjadala huo utaandaliwa katika ukumbi wa Karimjee, barabara ya Samora Machel, kivukoni, jijini Dar es Salaam tarehe hiyo 24 saa kumi na moja jioni.Miongoni mwa watakaokuwa wageni rasmi na viongozi wa mijadala hiyo ni pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dr Guido Herz, Mhariri mkuu wa DW, Marc Koch, mkuu wa idara ya matangazo ya lugha za Kiafrika na Mashariki ya Kati ya DW, Ute Schaeffer, mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, pamoja na waandishi wa habari mashuhuri huko Tanzania, Jenerali Ulimwengu, Tido Mhando, Ananilea Nkya, Ayoub Rioba na Majjid Mjengwa. DW imejitolea tangu zama kutoa habari za uhakika na zisizoegemea upande wowote kwa Bara la Afrika.Usikose kuhudhuria!!.

Mwandishi: Saumu Yusuf

Mhariri: Othman Miraji